Watu wengi huweza kutambua mataifa mbalimbali dunia kwa kuangalia kwenye bendera husika ya nchi hiyo. Hii imeifanya bendera ya nchi husik...
Watu wengi huweza kutambua mataifa mbalimbali dunia kwa kuangalia kwenye bendera husika ya nchi hiyo. Hii imeifanya bendera ya nchi husika kuwa alama kubwa ya utambuzi wa nchi.
Mara kadhaa utaona ndege, magari, viwanja, fedha na vitu vingine vya umma vikiwa vimechorwa bendera ya nchi husika kama alama ya utambuzi na kujitangaza.
Kwa upande mwingine, taifa huwa halitumii bendera tu kujitangaza bali hutumia mnyama kama alama ya utambuzi ya taifa hilo. Mataifa mbalimbali duniani hutumia mnyama mmoja kama mmanya wa taifa hilo ambaye huliwakilisha.
Mfano, mataifa kama Australia humtumia Kangaroo kama mnyama wa taifa, Ubelgiji hutumia Simba, Canada hutumia Farasi.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, hawa ndio wanyama wanaowakilisha mataifa ya mbalimbali Afrika Mashariki.
1. Tanzania
Mnyama anayeliwakilisha taifa la Tanzania ni Twiga. Kwa upande wa Tanzania picha imewekwa katika ndege za serikali, noti za fedha na maeneo mengine.
2. Kenya
Mnyama anayewakilisha taifa la Kenya ni Simba.
3. Uganda
Mnyama anayewakili taifa la Uganda ni Swala dume jamii ya Uganda.
4. Rwanda
Mnyama anayewakilisha taifa la Rwanda ni Chui.
5. Burundi
Mnyama anayewakilisha taifa la burundi ni Simba ambapo kwenye ndembo ya taifa hilo kuna kichwa cha Simba.