Waziri wa habari, mawasiliano, na teknolojia Joe Mucheru amesema ni lazima kuwepo mfumo wa zamani wa kuwasilisha matokeo ya uchaguzi utak...
Waziri wa habari, mawasiliano, na teknolojia Joe Mucheru amesema ni lazima kuwepo mfumo wa zamani wa kuwasilisha matokeo ya uchaguzi utakaotumiwa kwenye uchaguzi mkuu ujao, endapo mfumo wa kielektroniki utafeli. Akihojiwa na kamati ya seneti kuhusu sheria, Mucheru amesema mifumo yote miwili inapaswa kutumiwa ili kuzuia kuwepo changamoto zozote kwenye zoezi hilo.
Hata hivyo amekabiliwa na wakati mgumu alipodai huenda Alshabab ikadukua mitandao na kuathiri mfumo wa elektroniki utakaokuwa ukitumiwa.
Mucheru pia ameiambia kamati hiyo hitaji la kujumishwa kwa mfumo huo wa zamani, halitaathiri tarehe ya uchaguzi. Afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba naye amesema huenda ikalazimu shughuli hiyo kuendeshwa na kampuni itakayopewa kandarasi ya kusambaza vifaa vya BVR.
Kamati hiyo inayoongozwa na seneta Amos Wako, inakusanya maoni kuhusu mabadiliko ya sheria tata za uchaguzi kutoka kwa washika dau mbalimbali.

COMMENTS