Watoto wawili walio chini ya umri wa miaka mitano wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea moto katika kijiji cha Mwachome Mtaa wa P...
Watoto wawili walio chini ya umri wa miaka mitano wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea moto katika kijiji cha Mwachome Mtaa wa Patanani huko Matuga kaunti ya Kwale usiku wa kuamkia Jana.
Watoto wawili walio chini ya umri wa miaka mitano wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea moto katika kijiji cha Mwachome Mtaa wa Patanani huko Matuga kaunti ya Kwale usiku wa kuamkia jana.
Jawa Mwero mwenye umri wamiaka 2 na Omar Mwero wa miaka 3 walikuwa wamelala kabla ya nduguyao mwenye umri wa miaka 7 kuwasha taa ya koroboi ambayo iliteketeza makuti ya nyumba yao na kusababisha kisa hicho kutoka.
Akithibitisha kisa hicho Kamanda wa polisi kaunti ya kwale Kenenth Kimani amesema kwamba mama ya watoto hao alikuwa ameenda shughuli za kibiashara katika maeneo ya Likoni na baba yao pia hakuwa nyumbani wakati wa mkasa huo.
Miili yao imehifadhiwa katika chumba cha hifadhi ya maiti cha hospitali ya rufaa ya Msambweni huku uchunguzi ukianzishwa na maafisa wa usalama.

COMMENTS